عن أبي سعيدٍ الخُدريِّ رضي الله عنه، أن النبيَّ ﷺ قال:«لتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ مَن قَبْلَكم، شِبرًا بشِبرٍ، وذراعًا بذراعٍ، حتى لو سَلَكوا جُحْرَ ضَبٍّ لَسَلكْتموه»، قلنا: يا رسول الله، اليهود والنصارى؟ قال: «فمَن؟!»

Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

kwamba Mtume Rehma na Amani zimshukie amesema: 1- “Mtafuata njia za waliotangulia kabla yenu. 2- hatua kwa hatua, dhiraa kwa dhiraa, 3- Hata kama wangeingia kwenye shimo la mburukenge, nanyi mngaliingia.” 4- Tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni Mayahudi na Wakristo? Akasema Mtume Rehma na Amani zimshukie: "basi ni nani kama sio hao?! 

Abu Saeed Sa’d bin Malik

Ni: Abu Saeed Sa’d bin Malik bin Sinan Al-Ansari Al-Khazraji Al-Madani, Al-Khudri, sahaba mkubwa miongoni mwa mafakihi wa Maswahaba. Alidharauliwa na kudogeshwa siku ya vita vya Uhud, na baba yake aliuawa kishahidi katika vita hiyo. Kisha alishiriki vita kwa mara ya kwanza ilikuwa ni vita ya handaki, na akashuhudia pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie, vita kumi na mbili. Amesimulia Hadithi nyingi, na akatoa fatwa kwa muda, alifariki mwanzoni mwa mwaka wa sabini na nne [1]

Marejeo

1.  Tazama: “Tadhkirat al-Hafidh” cha al-Dhahabi (1/36), “Al-Isbah fi Tamayuz Maswahaba” cha Ibn Hajar (3/85), “Mwanzo na Mwisho” cha Ibn Kathir (9/3, 4), “Al-Tabaqat al-Kabeer” cha al-Zuhri (5/350) 



Miradi ya Hadithi