عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنِينَ أَنَّهَا قَالَتْ: "أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ مِنَ الوَحْيِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لا يَرَى رُؤْيَا إِلَّا جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الخَلاءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ - وَهُوَ التَّعَبُّدُ - اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ العَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ المَلَكُ فَقَالَ: اقْرَأْ، قَالَ: «مَا أَنَا بِقَارِئٍ»، قَالَ: «فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، قُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، فَقُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ:﴿اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ (1) خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ (2) اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ (3)﴾[العلق: ١ – ٣]»، فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ ﷺ يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، فَقَالَ: «زَمِّلُونِي زَمِّلُونِي» فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ. فَقَالَ لِخَدِيجَةَ وَأَخْبَرَهَا الخَبَرَ: «لَقَدْ خَشِيتُ عَلَى نَفْسِي».فَقَالَتْ خَدِيجَةُ: كَلَّا وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا:إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ،وَتَحْمِلُ الكَلَّ،وَتَكْسِبُ المَعْدُومَ،وَتَقْرِي الضَّيْفَ،وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الحَقِّ، فَانْطَلَقَتْ بِهِ خَدِيجَةُ حَتَّى أَتَتْ بِهِ وَرَقَةَ بْنَ نَوْفَلِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ العُزَّى، ابْنَ عَمِّ خَدِيجَةَ، وَكَانَ امْرءًا تَنَصَّرَ فِي الجَاهِلِيَّةِ، وَكَانَ يَكْتُبُ الكِتَابَ العِبْرَانِيَّ، فَيَكْتُبُ مِنَ الإِنْجِيلِ بِالعِبْرَانِيَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكْتُبَ، وَكَانَ شَيْخًا كَبِيرًا قَدْ عَمِيَ، فَقَالَتْ لَهُ خَدِيجَةُ: يَا بْنَ عَمِّ، اسْمَعْ مِنَ ابْنِ أَخِيكَ، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: يَا بْنَ أَخِي، مَاذَا تَرَى؟ فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ خَبَرَ مَا رَأَى، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: هَذَا النَّامُوسُ الَّذِي نَزَّلَ اللَّهُ عَلَى مُوسَى، يَا لَيْتَنِي فِيهَا جَذَعًا، لَيْتَنِي أَكُونُ حَيًّا إِذْ يُخْرِجُكَ قَوْمُكَ! فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «أَوَ مُخْرِجِيَّ هُمْ؟»، قَالَ: نَعَمْ، لَمْ يَأْتِ رَجُلٌ قَطُّ بِمِثْلِ مَا جِئْتَ بِهِ إِلَّا عُودِيَ، وَإِنْ يُدْرِكْنِي يَوْمُكَ أَنْصُرْكَ نَصْرًا مُؤَزَّرًا. ثُمَّ لَمْ يَنْشَبْ وَرَقَةُ أَنْ تُوُفِّيَ، وَفَتَرَ الوَحْيُ" متفق عليه.


Kutoka kwa Aisha, Mama wa waumini

(Radhi Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema:“Ufunuo na (wahyi) wa kwanza kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ulianza kwa kuota njozi njema usingizini, akawa kila anachokiota chochote basi kinatokea kama alivyoona usingizini.Kisha akapenda kujitenga,Na alikuwa anajitenga katika Pango la Hira, akifanya ibada masiku kadhaa, kabla ya kurudi katika familia yake, anaandaa akiba ya chakula kwa ajili yao, na kisha (akitaka kurudi kule pangoni) anaenda kwa Bi Khadija na anamuandalia akiba ya chakula (kwa kadiri ya masiku atakayokuwa akianya ibada).Mpaka akafunuliwa ufunuo (wahyi wa kwanza) akiwa ndani ya pango la Hiraa. Malaika Jibril akamjia na kusema: Soma. Akasema: “Mimi sijui kusoma”.Mtume (Rehma na Amani zimfikie) anasimulia mwenyewe kwa kusema: Basi (Malaika Jibril) akanishika na kuniminya mpaka nikachoka, kisha akaniachia na kuniambia: Soma, Nikasema: “Mimi sijui kusoma”. Kisha (Malaika Jibril) akanishika kwa mara ya pili na kuniminya mpaka nikachoka, kisha akaniachia. Na kuniambia: Soma, Nikasema: “Mimi sijui kusoma”. akanishika tena na kuniminya mpaka nikachoka, (alifanya hivyo) kwa mara ya tatu mpaka nikakosa nguvu kabisa. Kisha akaniachia na kusema: “Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba (1) Amemuumba mwanadamu kutokana na tone la damu (2) Soma! Na Mola wako Mlezi ni Mkarimu kushinda wote (3) [Al-Alaq: 1-3] (Baada ya hapo) Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimfikie) akarudi (akiwa na aya hizo za mwanzo kichwani) huku amejawa na woga, akaingia (nyumbani) kwa Bi khadija (Radhi za mwenyezi mungu zimfikie) akisema: “Nifunikeni jamaani, Nifunikeni” Wakamfunika hadi hofu ilipoisha.Mtume aka msimulia Bi Khadija kilichotokea, kisha akasema “Hakika naiogopea saana nafsi yangu”Bi Khadija akamwambia: Hapana (usiogope), Wallahi Mwenyezi Mungu hawezi kukufedhehesha.Kwani wewe Unatabia ya kuunga Udugu,Na kuwasaidia wanyonge (wasiojiweza).Na unajitolea kuwasaidia waliotingwa.Na unawakirimu wageni,Na unawasaidia watu katika kutatua matatizo.(Baada ya hapo) Bi Khadija akampeleka kwa kaka yake (mtoto wa baba mdogo wake) aliekuwa anaitwa Waraqah bin Nufal bin Asad bin Abdul Uzza, bwana huyu Alikuwa ni mnaswara (kisha akatoka na kuingia katika dini ya Nabii Mussa), na alikuwa anafahamu akuandika Kiebrania, basi akawa akiandika injili kwa lugha ya Kiebrania, na alifanya kazi hiyo muda mrefu na kuandika alichoweza kuandika, mpaka akazeeka na akapofuka macho.Khadija (alipomuendea mtu huyo) akamwambia: Ewe binamu yangu, msikilize mpwa wako (anachosema). Warqah akamwambia: Ewe mtoto wa ndugu yangu, umeona nini? Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimfikie) akamsimulia (habari za Malaika aliemtokea pangoni), Waraqah akamwambia: huyo ndio malaika (Jibril) aliemteremsha Mwenyezi Mungu kwa Nabii Mussa (Rehma na Amani zimfikie).Natamani ningelikuwa kijana zama hizo (za mtume wa mwisho), na nikawa hai wakati watu wako watakapokufukuza! (Nikashirika kukuhami).Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimfikie): “Hivi ni (kweli) Watanifukuza?” Akasema Waraqah: “Ndio, hakuna mtu yeyote aliyewahi kuja (na ujumbe) kama uliokuja nao wewe isipokuwa atafanyiwa uadui”.Na ikiwa itanidiriki siku (ya kudhiriri kwako nikiwa hai) basi nitapambana kukunusuru (hadi upate) ushindi mnono.Waraqah hakuchukua muda mrefu akawa amefariki, na wahyi ukawa umekata (kwa muda).”

Imepokelewa Na Bukhari na Muslim.

Miradi ya Hadithi