عن أبي هريرة رضي الله عنه، عن النبيِّﷺ قال:«مَن صلَّى صلاةً لم يَقرَأْ فيها بأُمِّ القُرآنِ فهي خِدَاجٌ – ثلاثًا - غيرُ تَمامٍ»،فقيلَ لأبي هُرَيْرةَ: إنَّا نكونُ وراءَ الإمامِ؟ فقال: اقرَأْ بها في نَفْسِكَ؛فإنِّي سَمِعْتُ رسولَ اللهِ ﷺ يقولُ: «قال اللهُ تعالى: قَسَمْتُ الصلاةَ بَيْني وبينَ عَبْدي نِصفَيْنِ، ولعَبْدي ما سألَ،فإذا قال العبدُ: {الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ} [الفاتحة: 2]، قال الله تعالى: حَمِدني عبدي، وإذا قال: {الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ} [الفاتحة: 3]، قال الله تعالى: أثنى عليَّ عبدي، وإذا قال: {مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ} [الفاتحة: 4]، قال: مجَّدني عبدي،فإذا قال: {إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ} [الفاتحة: 5]، قال: هذا بيني وبين عبدي، ولعَبْدي ما سَألَ،فإذا قال: {اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ (6) صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ} [الفاتحة: 6، 7]، قال: هذا لِعَبْدي، ولِعَبْدي ما سَألَ»


Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, kutoka kwa Mtume, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, amesema:

1. “Mwenye kuswali swala ambayo hakusoma ndani yake Mama wa Qur’an, basi swala hiyo haijatimia, kayasema maneno haya mara tatu. 2. Akaambiwa Abu Hurayrah: Hakika sisi tunakuwa nyuma ya imamu? Akasema: Isomee moyoni mwako. 3. Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Amesema Mwenyezi Mungu: Nimeigawanya Swala baina yangu na mja Wangu vipande viwili, na mja wangu atapata alichoomba. 4. Iwapo mja atasema: “Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote” [Al-Fatihah: 2], basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Mja wangu amenisifu, na ikiwa atasema: “Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.” [Al-Fatihah: 3], Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Amenisifu.” Akisema mja wangu "Mmiliki wa Siku ya Kiyama} [Al-Fatihah: 4] Anasema Mwenyezi Mungu:Mja wangu amenitukuza. 5. Akisema: “Wewe tunakuabudu na Wewe tunakuomba msaada” [Al-Fatihah: 5], Anasema: Haya ni baina Yangu na mja Wangu, na mja Wangu atapata analoliomba. 6. Akisema: “Tuongoze kwenye njia iliyonyooka (6), njia ya wale uliowaneemesha, si ya wale ambao wamewaghadhibikiwa, wala waliopotea. Mwenyezi mungu husema: Hili ni la mja wangu na atapata mja wangu kile alicho kiomba”

Miradi ya Hadithi