عن العِرباضِ بنِ ساريةَ قال: قام فينا رسولُ الله ﷺ ذاتَ يوم، فوعَظَنا موعظةً بليغةً، وَجِلَتْ منها القلوبُ، وذَرَفَت منها العيونُ، فقيل: يا رسول الله، وعظْتَنا موعظةَ مُوَدِّع، فاعهَدْ إلينا بعهدٍ، فقال: «عليكم بتقوى الله، والسمعِ والطاعة، وإنْ عبدًا حبشيًّا، وسترَوْنَ من بعدي اختلافًا شديدًا، فعليكم بسُنَّتي، وسُنَّة الخلفاء الراشدين المهديِّين، عَضُّوا عليها بالنَّوَاجِذ، وإيَّاكم والأمورَ المُحدَثاتِ؛ فإن كلَّ بِدعة ضلالة».

00:00
00:00
تحميل الملف الصوتي
00:00
00:00
تحميل الملف الصوتي

Kutoka kwa Al-Irbaadh bin Sariya, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

1- Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie alisimama kati yetu siku moja na kutuhutubia hotuba fasaha iliyozifanya nyoyo zitetemeke na macho kutoa machozi. 

2- Ikasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mawaidha yako ni mawaidha ya kuaga, basi tuusie . 

3- Akasema: “Juu yenu kumcha Allah. 

4- Kusikia na kutii, hata kama mtumwa wa Kihabeshi. 

5- Na mtaona ikhitilafu kali baada yangu. Ni lazima kushikamana na Sunnah zangu, na Sunnah za Makhalifa walioongoka, mzing’ang’anie kwa magego . 

6- Jihadharini na mambo mapya yaliyozushwa. Kwani kila uzushi ni upotofu.” 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu” .

[Al Imran: 102]

Na akasema Mola Mtukufu:

“Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”.

[An-Nisa: 59]

Na akasema Mola Mtukufu:

“Na anaye mpinga Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu”.

[Wanawake: 115]

Na akasema Mola Mtukufu:

“Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho.” .

[Al-Hashr: 7]

Miradi ya Hadithi