عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ بُسْرٍ، أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ شَرَائِعَ الإِسْلَامِ قَدْ كَثُرَتْ عَلَيَّ، فَأَخْبِرْنِي بِشَيْءٍ أَتَشَبَّثُ بِهِ، قَالَ: «لَا يَزَالُ لِسَانُكَ رَطْبًا مِنْ ذِكْرِ اللَّهِ».

Kutoka kwa Abdullah bin Busr Mwenyezi Mungu awe radhi naye.
1- Kwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika sheria za Kiislamu zimekuwa nyingi, basi niambie jambo moja nishikamane nalo .
2- Akasema: “Ulimi wako uendelee kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Basi nikumbukeni nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru” .
[Al-Baqara: 152]
Na akasema Allah aliyetukuka:
“Na mkumbuke Mola Mlezi wako nafsini kwako kwa unyenyekevu na khofu, na bila ya kupiga kelele kwa kauli, asubuhi na jioni. Wala usiwe miongoni wa walio ghafilika” .
[Al-A’raf: 205]
Mwenyezi Mungu amesema pia:
“Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua” .
[Ar-Ra'd: 28]
Akasema pia:
“Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda”.
[Al-Ankabut: 45]