عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «إِنَّ الدِّينَ يُسْرٌ، وَلَنْ يُشَادَّ الدِّينَ أَحَدٌ إِلَّا غَلَبَهُ، فَسَدِّدُوا وَقَارِبُوا، وَأَبْشِرُوا،وَاسْتَعِينُوا بِالْغَدْوَةِ وَالرَّوْحَةِ وَشَيْءٍ مِنَ الدُّلْجَةِ»


Kutoka kwa Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, amesema:

1- “Dini ni rahisi, 

2- Hakuna atakayeifanya dini kuwa ngumu ila itamshinda. 

3- Basi semeni kweli na muwaite watu karibu. 

4- Na toeni bishara njema. 

5- Na tafuteni msaada asubuhi na mchana na nyakati za usiku.” .

Muhtasari wa Maana

Mtume Rehma na Amani zimshukie anabainisha kuwa Dini ya Uislamu ni rahisi kuichukua, kwa sababu ya wepesi wa hukumu zake na urahisi wa gharama zake, na kwamba mwenye kuifanya dini kuwa gumu, mtu huyo anataka dini hiyo imshinde kuiingia, na atakuwa hana uwezo na atakatiliwa mbali, hivyo Muislamu anatakiwa kuwa na bidii na na kuwa nayo karibu. Na alitubashiria mtume kwa malipo makubwa kwa kuifuata dini hiyo.

Kisha akaeleza kuhusu nyakati bora za ibada na unyenyekevu, ambazo ni mwanzo wa mchana na mwisho wake na mwisho wa usiku.

Miradi ya Hadithi