41 - KUJIEPUSHA NA KURTADI, UKAFIRI, NA SHIRKI KUBWA

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ قَالَ: «بَادِرُوا بِالْأَعْمَالِ فِتَنًا كَقِطَعِ اللَّيْلِ الْمُظْلِمِ، يُصْبِحُ الرَّجُلُ مُؤْمِنًا وَيُمْسِي كَافِرًا، أَوْ يُمْسِي مُؤْمِنًا وَيُصْبِحُ كَافِرًا، يَبِيعُ دِينَهُ بِعَرَضٍ مِنَ الدُّنْيَا» 

Kutoka kwa Abuu Hurairah, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na

Amani ziwe juu yake) amesema: “Jitahidini kufanya matendo mema, kwa sabubu kuna fitina kama kiza cha usiku totoro, Mtu anaamka akiwa ni muumini, jioni anakuwa kafiri, au jioni anakuwa ni muumini, asubuhi kafiri, Anaiuza dini yake kwa mapambo ya Dunia.


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu”

[Al Imran: 133]


Na akaseme Mkuu na Mtukufu:

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu”.

[Al-Anfal: 25]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi mlio amini! Isikudanganyeni mali yenu, wala watoto wenu, mkasau kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio walio pata hasara kubwa (9) Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Mola wangu Mlezi! Naomba unicheleweshe japo muda kidogo nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema (10) Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapo fika muda wake wa kifo; na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda (11)’’

[Al-Munafiqun: 9-11]

Miradi ya Hadithi